UTENDAJI WA WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA KUPIMWA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inakusudia kupima utendaji wa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwa kutumia viashiria muhimu hususan usimamizi wa mapato na makusanyo ya ndani pamoja na upelekaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo. Amesema watendaji hao pia watapimwa  kwa namna wanavyosimamia mikopo ya asilimia 10 ikiwa ni pamoja na marejesho, usimamizi wa miradi ya maendeleo na uzuiaji